Rais Magufuli Asema Hataingilia Mgogoro wa Zanzibar,Ataka Wenye Malalamiko Waende Mahakamani….Hotuba Nzima Ya Rais Iko Hapa
Filed Under:
Habari mix,
Videos
Unknown
Rais John Magufuli jana alitumia dakika 55 kuzungumza na wazee wa Dar es Salaam, akigusa kila sekta wakati akizungumzia mambo aliyoyafanya katika siku 100 na anayotarajia kufanya.
Katika hotuba hiyo ambayo aliendelea kuzungumzia jinsi nchi inavyotafunwa, kiongozi huyo wa Serikali ya Awamu ya Tano aliweka msimamo wake kuhusu mgogoro wa kisiasa Zanzibar, akisema hataingilia.
Pia alidokeza kuhusu uteuzi wa wakuu wa mikoa na wilaya, akimhakikishia Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda kuendelea au kupandishwa cheo.
Mambo mengine aliyozungumzia ni mafanikio na changamoto ya elimu bure, ujenzi wa barabara na madaraja, utendaji wa mawaziri, miradi ya umeme, huduma kwenye Hospitali ya Muhimbili, vyombo vya habari, na kuwataka wananchi wajitathmini wamefanya nini katika siku 100 za kwanza za utawala wake.
Dk Magufuli aliyekuwa ameambatana na Makamu wa Rais, Samia Suluhu, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Naibu Spika Dk Tulia Ackson, alikuwa akizungumza na baraza la wazee wa Dar es Salaam kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, ikiwa ni siku yake ya 102 tangu alipoapishwa Novemba 5, 2015 kuwa Rais.
Mkutano huo ulihudhuriwa na watu zaidi 3,000, wakiwamo mawaziri, viongozi wa CCM na viongozi wa dini, walioongozwa na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaj Mussa Salum na Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima.
Rais Magufuli aliyeingia katika ukumbi huo saa 8:30 mchana, alianza kuzungumza saa 9:36 alasiri na kumaliza saa 10:32 jioni, akisisitiza wananchi wamuombee aweze kutekeleza majukumu yake, ikiwa ni pamoja na kutumbua majipu.
Uchaguzi Zanzibar
Rais ambaye amekuwa kimya kwa muda mrefu kuhusu mgogoro wa kisiasa Zanzibar, hatimaye jana aliweka bayana msimamo wake akisema hataingilia kwa kuwa anaheshimu utawala wa sheria.
Rais ambaye amekuwa kimya kwa muda mrefu kuhusu mgogoro wa kisiasa Zanzibar, hatimaye jana aliweka bayana msimamo wake akisema hataingilia kwa kuwa anaheshimu utawala wa sheria.
“Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) ni huru kwa mujibu wa Kat iba ya Zanzibar kifungu kati ya 112 au 115. Lakini kama ilivyo kawaida Tume huru ya uchaguzi duniani haiwezi kuingiliwa na rais yoyote. Ni kama ilivyo ZEC na (Tume ya Taifa ya Uchaguzi) NEC ndivyo ilivyo,” alisema Rais.
Alisema uamuzi wa ZEC kufuta uchaguzi Zanzibar na kisha kutangaza tarehe ya marudio, hauwezi kuingiliwa na mtu yeyote, akisisitiza kuwa wanaotaka tafsiri ya kisheria juu ya uamuzi wa ZEC, waende mahakamani.
“Mahakama ipo hutaki kwenda halafu unasema Magufuli ingilia! Nenda mahakamani ukapewe tafsiri ya haki. Siingilii na nitaendelea kukaa kimya. Jukumu langu ni kuhakikisha usalama wa Zanzibar, Pemba na Tanzania unaimarika,” alisema.
“Ukifanya “fyokofyoko” katika eneo lolote nchini, utashughulikiwa na vyombo vya ulinzi na usalama.”
Mgogoro wa kisiasa Zanzibar uliibuka baada ya ZEC kufuta matokeo ya uchaguzi wa rais, wawakilishi na madiwani kwa maelezo kuwa sheria na kanuni zilikiukwa na baadaye kutangaza Machi 20 kuwa siku ya kupiga kura upya.
Wakati mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salim Jecha akitangaza kufuta matokeo siku ambayo alitakiwa amtangaze mshindi wa kiti cha urais, tayari matokeo ya majimbo 31 yalikuwa yameshatangazwa huku majimbo tisa yakiwa yameshahakikiwa. Pia washindi wa viti vya uwakilishi na udiwani walishatangazwa na kupewe hati za ushindi.
Chama kikuu cha upinzani Zanzibar, kimepinga ZEC kufuta matokeo kikisema ni kukiuka katiba kwa kuwa ushindi unapingwa mahakamani tu na kimejitoa kwenye uchaguzi wa marudio huku kikimtaka Rais Magufuli aingilie katika kutatua mgogoro huo mezani.
“Sitaingia suala la Zanzibar,” alisema Magufuli.
Akizungumzia mabadiliko ambayo Serikali yake inayafanya, Rais alisema yana changamoto zake ambazo zinaweza kuwagusa baadhi ya watu, lakini akasema watakaoguswa ni wachache kwa faida ya wengi.
“Tanzania haitakiwi kuwa na wanafunzi wanaokaa chini, watu kukosa maji, Muhimbili watu kulala watano kitandani. Tanzania hii ina neema ila lazima tutambue wapo watu wachache waliotufikisha hapa,” alisema.
Alisema mabilioni ya fedha za Watanzania yanatumika hovyo.
“Ifike mahali Watanzania tujiulize tumemkosea nini Mungu? kwa nini asitusamehe kwa makosa tuliyoyafanya. Serikali imejitoa sadaka kwa ajili ya Watanzania,” alisema.
“Ndani ya Serikali tumejipanga, anayetaka kutukwamisha tutambomoa kwa faida ya Watanzania, hasa wanyonge. Haiwezekani kila mahali unapokwenda ukute wananchi wanalia wakati nchi ina rasilimali za kila aina.”
Ufisadi
Katika hotuba yake ambayo mara kwa mara alikuwa ikikatishwa na shangwe za wananchi, Dk Magufuli alianza kuzungumzia ufisadi, akisema katika siku 100 ambazo amekaa madarakani, wamejifunza mengi na kukumbana na changamoto lukuki.

“Wapo watu katika nchi hii kwao fedha sio tatizo, fedha hizo hawajazipata kwa uhalali wamezipata kutoka kwa masikini wanaohangaika . Kila tulipokuwa tunagusa kuna maajabu,” alisema
Alisema alimtuma Majaliwa kwenda bandarini na Katibu Mkuu wa Tamisemi kwenda wilayani Bariadi na wakakumbana na madudu.
“Akiwa Bariadi alikuta barabara ya kilomita moja imejengwa kwa Sh2 bilioni tena ni barabara ya halmashauri ya wilaya. Mimi nimekaa Serikalini sijawahi kujenga barabara kuu ya kilomita moja kwa Sh2 bilioni, ila hii ya halmashauri imejengwa kwa kiasi hicho?” alihoji.
“Barabara ya kilomita nne na nusu ya Halmashauri ya Bariadi imejengwa kwa Sh9.2 bilioni, wakati mkuu wa mkoa, wilaya, mkurugenzi na mhandisi yupo.
“Ninapozungumza kutumbua majibu, Watanzania mtuunge mkono tuyatumbue kwelikweli.”
Alisema kiwango hicho cha fedha kingeweza kutengeneza kilomita 22 hadi 23 za lami.
Wizi bandarini
Akizungumzia wizi wa mafuta bandarini alieleza kushangazwa na kitendo cha mita za mafuta kutofanya kazi kwa miaka mitano.
Akizungumzia wizi wa mafuta bandarini alieleza kushangazwa na kitendo cha mita za mafuta kutofanya kazi kwa miaka mitano.
“Waziri Mkuu alikwenda bandarini na kukuta flow meter ya kupimia mafuta yanayoingia nchini haifanyi kazi kwa miaka mitano,” alisema.
“Mafuta yanaingia nchini yanagawiwa kwa watu na ndiyo maana mnaona kutoka Dar es Salaam kwenda Kibaha kila mahali kuna sheli (vituo vya mafuta).”
Kutokana na wizi huo wa mafuta, juzi Majaliwa alimsimamisha kazi mtendaji mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA) na meneja wake wa kitengo cha bandari kupisha uchunguzi.
Alisema fedha ambazo zingepatikana kama mafuta hayo yangepimwa na kulipiwa kodi zingeweza kutumika kununua dawa hospitali, kusomesha wanafunzi bure na kujenga barabara.
“ Hiyo ndiyo Tanzania tuliyoikuta sisi. Mifano ni mingi ya kila aina,”alisema.
Madudu muhimbili
Alisema alitembelea Muhimbili na kusimamishwa na akinamama waliomtaka aende wodi ya wanawake, lakini wasaidizi wake wakamzuia.
Alisema alitembelea Muhimbili na kusimamishwa na akinamama waliomtaka aende wodi ya wanawake, lakini wasaidizi wake wakamzuia.
“Walinizuia ila nilikataa. Niliwambia naenda hukohuko na niliyoyakuta ni maajabu,” alisema.
Alisema katika wodi namba 36, alikuta maji kutoka chooni yanavuja huku akina mama wakiwa wamelala chini, watano kwenye godoro moja.
“Ukiwa unaenda Muhimbili jirani kuna jengo la ghorofa tatu, linatumika kama ofisi ya uzazi na watoto. kuna wafanyakazi 70. Ukisogea mbele zaidi kuna jengo lilianza kujengwa tangu utawala wa Serikali ya Awamu ya Pili mpaka leo halijaisha,” alisema.
“(Rais wa Serikali ya Awamu ya Pili, Ali Hassan) Mwinyi hakulimaliza, akaja (wa Awamu ya Tatu, Benjamin) Mkapa hakulimaliza, akaja (wa Awamu ya Nne, Jakaya) Kikwete hakulimaliza na sasa nipo mimi bado halijaisha.”
Alisema inashangaza kuona viongozi wa hospitali hiyo wakishindwa kumfukuza mkandarasi anayejenga jengo hilo ambaye ni Masasi Construction Engineering .
Alisema alipokuwa Waziri wa Ujenzi alifukuza makandarasi 3,000, lakini akashangazwa kuona jengo la ghorofa nne likijengwa zaidi ya miaka 20.
“Nadhani jengo hili limeweka rekodi duniani,” alisema.
Alisema jengo hilo likimalizika linaweza kuchukua watu 342, lakini hivi sasa lina watu 100, waliopo eneo la chini la ghorofa hilo, halina umeme wala maji.
Alisema Muhimbili kuna jengo la Taasisi ya Tiba ya Mifupa ya Muhimbili (Moi), kuna jengo la ghorofa sita lililoanza kujengwa miaka minne iliyopita, lakini mpaka leo halijamalizika kutokana na mvutano kati ya Moi na mkandarasi anayetaka kulipwa Sh9 bilioni.
“Wamechukua wagonjwa wachache na kuwaweka ghorofa ya kwanza hadi ya tatu. Lina jenereta ila haijafungwa. Hiyo ndiyo Tanzania,” alisema.
Alisema ameshatoa maagizo kwamba ndani ya siku mbili wafanyakazi hao 70 waondolewe kwenye jengo hilo linalotumika kama ofisi na badala yake viwekwe vitanda vya wagonjwa.
“Sasa Waziri wa Afya na Katibu Mkuu watajua watawatafutia wapi pa kuwapeleka. Wanaweza kuwapeleka pale wizara ya Afya wakakae nao huko. Ndani ya siku mbili hizohizo ofisi hiyo ijae vitanda na akina mama waliokuwa wanalala chini wahamishiwe kwenye jengo hilo,” alisema.
Alisema ili Tanzania isiwe ombaomba lazima viongozi wajifunze kutokukubali kulea makosa.
“Kama ni majipu tutayatumbua kwelikweli. Likienda kichwani tutalitumbua, likienda kifuani tutalitumbua, likienda mgongoni tutalitumbua ili mradi majipu yaishe na Tanzania iende mbele,” alisema.
Tanzania bila mapato haiwezekani
Alisema Tanzania haiwezi kuendelea bila kuwa na mapato yake.
Alisema Tanzania haiwezi kuendelea bila kuwa na mapato yake.
“Wafanyabiashara wamekuwa wakikwepa kulipa kodi. Mara ya kwanza tulipoanza kuchukua hatua tulipata zaidi ya Sh1 trilioni, mwezi uliofuata tulipata Sh1.592 trilioni na Januari tulikusanya Sh1.063 trilioni,” alisema.
Alisema Serikali ya Awamu ya Tano inataka kuona fedha hizo zikiwahudumia wananchi masikini.
“Zipo kejeli nyingi, wanasema ni nguvu ya soda. Hata kama ni soda ukiweka gongo utalewa. Hii ni soda ‘special’ ambayo tumedhamiria kufanya kazi kwa ajili ya Watanzania. Haiwezekani nchi tajiri kama Tanzania tuwe ombaomba, inatakiwa iwe inaombwa misaada,” alisema.
Aliwataka Watanzania kujenga utamaduni wa kulipa kodi na kudai risiti kwa kila manunuzi wanayoyafanya.
Kukwama kwa mradi wa umeme
Kuhusu mradi wa umeme wa gesi wa Kinyerezi 2 uliokwama tangu mwaka 2012, alisema wafadhili kutoka Japan walitoa dola 292 za Marekani na Serikali ya Tanzania ilitakiwa kuchangia asilimia 15 ya fedha hizo.

Alisema mradi huo utaingiza zaidi ya megawati 240 za umeme.
“Fedha hizo tumezitoa na kampuni kutoka Japan imeshaanza kazi na mwezi ujao tunakwenda kuweka jiwe la msingi. Mradi wa ujenzi wa barabara ya juu Dar es Salaam mkandarasi ameshaanza kazi na fedha za awali ameshalipwa,” alisema.
Alisema upembuzi yakinifu wa mradi wa barabara ya njia sita kutoka Dar es Salaam kwenda Chalinze, umeshamalizika na kuna kandarasi zaidi ya 12 wameshaomba zabuni.
“Katika kipindi hikihiki cha awamu ya tano itajengwa ili tuwe na barabara ya njia sita kupunguza msongamano wa magari,” alisema.
Rais pia alidokeza kuhusu mradi wa ujenzi wa daraja la urefu wa kilomita saba litakalopita baharini kutoka ufukwe wa Coco hadi Hospitali ya Aga Khan, akisema Serikali imeshapata zaidi ya Sh260 bilioni.
“Kuhusu barabara ya Mbagala rangi tatu kuja mjini (Posta), nilikuwa nazungumza na ubalozi wa Japan wapo katika utaratibu wa kutangaza tenda,” alisema.
Pia alizungumzia ujenzi wa barabara za juu zitakayojengwa kwenye makutano ya Ubungo.
Alisema makutano hayo yatakuwa na ghorofa tatu ambazo zitakuwa na barabara zinazokutana eneo hilo ili kuondoa tatizo la foleni.
“Benki ya Dunia imekubali kutoka Sh67 bilioni kujenga interchange (mzunguko wa juu wa barabara) ya ghorofa tatu pale Ubungo, nina uhakika watani zangu wazaramu watakwenda pale kufunga ndoa,” alisema.
Kuifufua ATCL
Alisema Serikali ina mpango wa kufufua Shirika la Ndege (ATCL), ambalo hivi sasa lina ndege moja lakini limeajiri wafanyakazi 200.
Alisema Serikali ina mpango wa kufufua Shirika la Ndege (ATCL), ambalo hivi sasa lina ndege moja lakini limeajiri wafanyakazi 200.
Alisema kwa sasa wanakusanya fedha za kutosha ili kuweza kununua ndege aina ya Airbus yenye uwezo wa kuchukua kuanzia abiria 120 na kuendelea, akisema bei yake ni takriban Sh140 bilioni.
“Mkijipanga mnaweza kuwa mnanunua ndege moja kila mwezi,”alisema.
Elimu bure
Akizungumzia changamoto ya elimu bure alisema wanafunzi walioanza darasa la kwanza nchini mwaka huu ni 1,337,000, jambo ambalo alisema linaonyesha kuwa wananchi walikuwa wakishindwa kuwapeleka watoto wao shule kwa sababu ya kukithiri kwa michango.

Alisema changamoto zilizojitokeza baada ya Serikali kuanza kutoa elimu bure watazimaliza, ikiwa ni pamoja na kutenga fedha nyingi zaidi kwa ajili ya kuzipeleka katika shule.
Aliwashukuru wananchi ambao wameanza kujitokeza kuchangia ujenzi wa madarasa na kumsifu Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni kwa kuendesha harambee ya kuchangia ujenzi wa shule.
Awashukia wakuu wa mikoa na wilaya
Dk Magufuli pia alizungumzia utendaji wa wakuu wa wilaya na mikoa na wakurugenzi wao, akiwataka kutathmini hali ilivyo kwenye shule na ofisi zao.
Dk Magufuli pia alizungumzia utendaji wa wakuu wa wilaya na mikoa na wakurugenzi wao, akiwataka kutathmini hali ilivyo kwenye shule na ofisi zao.
“Kama unajua kujipima vizuri, ujitambue kuwa hutoshi kuwa kiongozi. Sijateua wakuu wa mikoa, wakuu wilaya na wakurugenzi ili niendelee kuwachambua vizuri (waliopo) ni nani anatosha na nani hatoshi,” alisema..
“Kutosha kwao ni lazima wajipange watatatua vipi kero za wananchi. Lazima ifike mahali viongozi tujue jukumu letu. Unapopewa jukumu la uongozi wewe ni mwakilishi wa wanyonge.”
Huku akiwataka Watanzania wa kada zote nao kujipima walichoifanyia nchi ndani ya siku 100, alisema haingii akilini kiongozi kusimama na kusema chakula hakuna wakati mvua inanyesha kila mkoa nchini.
“Kiongozi umeshindwa hata kuhamasisha watu walime. Natoa wito kwa viongozi wenzangu. Katika mkoa, wilaya au tarafa itakayokuwa haina chakula kwa mwaka huu ambao mvua inanyesha, ajitambue hafai kuongoza katika nchi,” alisema.
Alisema aliahidi kuwalipa wazee waliolitumikia taifa lakini jambo hilo haliwezekani kama kutakuwa na vijana wanaoshinda mitaani bila kufanya kazi.
“Najua mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, wakuu wa mikoa wenzako watakuuliza nitateua lini wakuu wa mikoa na wilaya. Kwanza tarehe ya kuteua hawataijua na ninaendelea kuwachambua,” alisema Magufuli.
“Lakini angalau Makonda umeshajihakikishia walau utakuwepo ila na wewe usiende kulala, endelea kufanya juhudi. “Ukipanda cheo watu wasikuonee wivu.”
Alisema Makonda amejijengea heshima kubwa kwa kuhamasisha watu wa kada mbalimbali kumaliza changamoto za kuongezeka wa wanafunzi, uhaba wa madarasa na madawati.
Kuhusu changamoto za elimu bure, Rais alisema asilimia 80 ya viongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano wanaishi Dar es Salaam, akiwamo yeye, waziri mkuu, mawaziri, makatibu wakuu na naibu spika.
“Wao wakitoa milioni moja moja zinafika milioni 82 na zitabaki milioni 18, lakini kuna Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na mimi. Tuigawane hii na kila mmoja achangie Sh6 milioni itimie Sh100 milioni na tutaileta kwenye uongozi wa mkoa wa Dar es Salaam,” alisema.
Alisema kwa mamlaka aliyonayo ataongeza Sh2 bilioni na kumtaka mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kutozitumia vibaya, akitaka zigawanywe kwa kila wilaya ili zijengwe shule za kutosha kufidia wanafunzi wanaokaa chini.
Afagilia vyombo vya habari
Kiongozi huyo wa Serikali ya Awamu ya Tano pia alizungumzia vyombo vya habari ambavyo alisema vimefanya kazi kubwa na kuisaidia Serikali.
Kiongozi huyo wa Serikali ya Awamu ya Tano pia alizungumzia vyombo vya habari ambavyo alisema vimefanya kazi kubwa na kuisaidia Serikali.
“Hata sisi huwa tunafuatilia. Mfano katika gazeti la Jamhuri waliweka michoro fulani mpaka sisi (Serikali), tukajiuliza wamejuaje tunachotaka kukifanya?” alisema.
ANGALIA VIDEO HAPA CHINI
Polepole: CCM Haina Mpinzani
Filed Under:
Habari mix,
Siasa
Unknown
Alikuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba na Mwanaharakati, Humphrey Polepole, amesema CCM ndiyo chama pekee cha siasa nchini chenye misingi ya kuwatumikia wananchi ukilinganisha na vyama vingine vya siasa.
Alisema Jimbo la Iringa Mjini halikupaswa kwenda upinzani hivyo aliwataka viongozi wa CCM mkoani humo kujitathimini na kuona wapi walipoanguka ili waweze kulirudisha mwaka 2020.
Polepole aliyasema hayo jana wakati akifungua Kongamano la Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu la CCM mkoani humo.
Aliongeza kuwa, utendaji mzuri wa Serikali ya Rais Dkt. John Magufuli katika kutekeleza Ilani ya CCM, umedhihirisha wazi aina ya wana CCM ambao ni hazina wanaoweza kuleta maendeleo makubwa kwa jamii na nchi kwa ujumla.
Aliwataka wana CCM mkoani humo, kuanza kueleza mambo mazuri yanayofanywa na Rais Dkt. Magufuli katika utekelezaji wa Ilani ya CCM.
Polepole alisema kinachofanywa na Rais Dkt.Magufuli juu ya kuwatumikia Watanzania, kimewafanya wananchi watambue hazina kubwa iliyopo ndani ya CCM.
"Katika Uchaguzi Mkuu 2015, CCM ilipata ushindi wa asilimia 58 ambao si mzuri sana tunaoweza kujivunia...nguvu iongezwe zaidi ili tupate ushindi wa asilimia 80 hadi 88.
"Njia pekee ya kuongeza ushindi wa CCM, lazima tufanye kazi ya kukijenga chama," alisema Polepole
Mapigano ya wakulima na wafugaji yaibuka tena mvomero
Filed Under:
Habari mix
Unknown
zaidi ya mbuzi na kondoo 200 huko morogoro wilaya ya mvomero kijiji cha dihinda wamekatwa katwa na walinzi wa jadi kutoka Gairo wanaojulikana kwa jina la Mwanu
Taarifa zinasema kuwa mifugo hiyo ilikula nusu hekari ya mazao ya mkulima mmoja kijijini hapo na taarifa ziliwafikia walinzi hao ambapo walifika na kukatakata hiyo mali ya mama mmoja mjane mfugaji wa jamii ya kimasai
Lakini inadaiwa kuwa mifugo ya mama huyo haikuhusuka kula mazao hayo bali ni mifugo ya mfugaji mwingine ndio iliyohusika
waziri mwenye dhamana kupitia wizara ya mifugo na kilimo hivi sasa ameelekea eneo la tukio
Nuhu Mziwanda Afunguka ' Shilole Hakuwa Mke Mzuri Kwangu Ndio Maana Nimefuta Tattoo yake'
Msanii Nuh Mziwanda amefunguka baada ya kuachana na mwandani wake Shilole, na kusema kuwa Shilole hakuwa mtu mzuri kwake, ndiyo maana ameamua kufuta hata tatoo ya jina lake aliyoichora.
Nuh ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, na kusema kwamba wakati yupo kwenye mahusiano na Shilole alishindwa kuonesha undani wake, ambao amekuja kuujua baada ya kuachana na penzi kuisha.
“Baada ya mapenzi kuisha mi nimekuwa adui yake, amehack acount yangu ya instagram najaribu kuwacheki wa kurudisha acount yangu wanashindwa kunirudishia anabana kila sehemu, kuna vitu ananifanyia vidogo vidogo ambavyo nimefanya kugundua kuwa hakuwa mwanamke mzuri kwangu, alikuwa anashindwa kuonesha true colour yake nimekuja kuijua baada ya kuachana naye”, alisema Nuhu.
Pia Nuh Mziwanda amesema iwapo wangeachana kwa amani na Shilole asingelazimika kuifuta tatoo hiyo, kwani ni ukweli usiopingika kwamba amemsaidia katika maisha yake.
“Mi ningeiacha tatoo kama Shishi ningeachana nae poa, kila mtu na maisha yake fresh tukionana tunasalimiana hakuna noma, lakini mwenzangu kwenye interviews anasema, akiitwa kwenye interview anaongea hiki kwamba mimi sina kitu, sijui nashindwa kusurvive nakula magengeni, anaongea vitu vingi ambavyo anajaribu kutoa fan base yangu, angekuwa mtu mzuri baada ya kuachana naye tatoo ningeiacha kwa sababu ningejua bado kabaki kuwa rafiki yangu na ni mtu ambaye alinisaidia”, alisema Nuh.
Pamoja na hayo Nuh amesema yeye binafsi hana chuki na msanii huyo ambaye alikuwa naye kwenye mahusiano, na kwa sasa ana mahusiano mengine ambayo asingependa kuyaweka wazi.
Mimi sina ubaya na Shishi , sina ugomvi naye na wala sitaki kufikiria kuja kuwa na bifu naye, nipo kwenye mahusiano lakini siwezi kuweka wazi mahusiano kwenye mitandao ya kijamii, sababu ni mke wangu yuko kwenye moyo wangu, hayupo instagram wala kwenye mitandao ya kijamii”, alisema Nuh.

Salam Jabir Nae Aibuka Kwenye Malumbano ya Video Mpya ya Ali Kiba Baada ya Baadhi Kuiponda...Asema Haya
Filed Under:
Habari mix,
Udaku
Unknown
Mtangazaji wa kipindi cha Mkasi ambacho kinarushwa kupitia ting'a namba moja kwa vijana (EATV) Salama Jabir amefunguka na kuwataka watanzania kuthamini na kuheshimu watu ambao wanajituma kufanya mambo katika kazi zao.
Salama amesema kuwa kazi ya msanii siku zote ni sanaa ambayo unaweza kuipenda au kutoipenda.
Salama Jabir amesema hayo kupitia Account yake ya Twitter kufuatia baadhi ya maoni ya mashabiki ambao wamekuwa wakiwaponda wasanii wa bongo pindi wanapokuwa wanatoa kazi zao hususani video huku mashabiki wengine wakienda mbali na kuponda au kuzungumzia jambo kama wao wana maarifa ya jambo hilo.
Imekuwa ni kawaida kwa mashabiki kuponda kazi za wasanii na kuwatusi kupitia mitandao yao ya kijamii jambo ambalo linakuwa linakatisha tamaa baadhi ya wasanii na kuwaumiza kwani maneno ambayo mashabiki huwa wanatumia ni makali na ya kukatisha tamaa.
Hali hii mara nyingi imekuwa ikisababishwa na makundi ya mashabiki maarufu kama Team, kuna watu wanaweza kuponda jambo ili mradi tu kwa sababu yeye si shabiki wa msanii fulani na wapo wengine wanafanya hivyo kwa lengo ya kukomesha, huku wengine wakitaka wasanii waendelee kuleta video za aina fulani pekee na ukifanya vinginevyo wanaona umekosea kwa sababu ndicho kitu walichozoea kifupi hawataki kukutana na kitu cha iana mpya.

"Kazi ya msanii ni Sanaa... Usingiingilie!! ni aidha utaipenda au hutaipenda simple!! Kama rahisi fanya na wewe tuone Respect kwa wanaojituma" Amesema Salama