Picha ya waziri wa kilimo na mifugo na mbunge wa Iramba Masharili Imezua "Hisia" Tofauti na mijadala mitandaoni. Picha hiyo inamuonyesha mwigulu nchemba akiwa na mwanae wa kiume na 'Caption' ya picha inayosomeka elimuniufunguo Kikubwa kilichozua mjadala ni nembo katika fulana ya mtoto yenye maandishi ya FEZA SCHOOL.
Maswali na mijadala ya wengi ni kuwa, Itakuwaje na moyo wa kuimarisha elimu katika shule za umma kama sehemu ya mawaziri ambao ni watekelezaji wa sera ya elimu bure na uboreshaji wa elimu katika shule za umma wana kimbiza watoto wao katika shule binafsi?Kwanini mawaziri ambao ni sehemu ya utekelezaji wa sera wanaoamini katika elimu bora katika shule za umma wao hawawapeleki watoto wao huko?
Picha hii imezua mijadala tofauti tofauti na wapo wanaoona Mh. Mwigulu yupo sahihi kupeleka watoto shule binafsi sababu ukweli ni kuwa shule za serikali elimu yao ni duni na isiyo na ushindani.
Hivyo mawaziri kuwapeleka watoto wao shule binafsi na zenye ubora kama FEZA SCHOOL ni kuwaepusha na elimu duni inayotolewa na serikali
Toa maoni yako hapo chini

Post a Comment